Wednesday, May 25, 2016

JOSE MOURINHO AKUBALI MASLAHI BINAFSI KUTUA OLD TRAFFORD, MKATABA WA MIAKA 3

Jose Mourinho takes an evening stroll on Tuesday evening ahead of his move to Manchester UnitedMazungumzo ya kumthibitisha Jose Mourinho kuwa Meneja mpya wa Manchester United yanaingia Siku ya Pili Jijini London huko England ambako Wakala wake Jorge Mendes, Mourinho mwenyewe na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Woodward, wanakutana.
Ripoti zimedai Mourinho, ambae atamrithi Louis van Gaal, alieondolewa Juzi, ameshakubali Urefu wa Mkataba na Maslahi yake binafsi lakini kikwazo kikubwa kinachochelewesha Dili kukamilika na Mkataba kusainiwa ni mgongano wa Umiliki wa Haki za Matangazo na Picha.
Pande hizo mbili zina Mikataba ya Kibiashara ambayo ni tofauti ambayo lazima yafikiwe makubaliano ili kusiwe na mgongano wa kimaslahi.

Mourinho (right) was accompanied by a security guard as he wandered around Central London Kwa mfano, wote, Man United na Mourinho, wako chini ya udhamini wa Kampuni ya Vifaa vya Michezo Adidas huku Mourinho akiwa Balozi wao na Man United wana Mkataba wa Miaka 10 na Kampuni hiyi wa thamani ya Pauni Milioni 750 ambao ulianza 2015.
Lakini yapo maeneo kadhaa yenye mgongano na moja ni Mkataba wa Mourinho na Kampuni ya Magari ya Jaguar wakati Man United wana Mkataba wa Miaka 7 Kampuni ya Magari ya General Motors ambayo Gari yao aina ya Chevrolet nembo yake hubebwa kwenye Jezi za Man United.

Hata hivyo, inaaminika mazungumzo hayo yatakamilika Leo na tamko rasmi kutolewa.