Thursday, May 26, 2016

JOSE MOURINHO KIMEELEWEKA OLD TRAFFORD! KUTEULIWA MENEJA MPYA MANCHESTER UNITED LEO IJUMAA

MENEJA wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Jose Mourinho ameteuliwa rasmi kuwa Meneja mpya wa Manchester United.
Mazungumzo kati ya upande wa Mourinho na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward yamekamilika hivi punde Jijini London.
Mourinho amekuwa hana kibarua tangu Desemba alipoondoka Chelsea na anambadili Louis van Gaal alietimuliwa Jumatatu iliyopita ikiwa ni Siku mbili tu baada ya kuiongoza Man United kutwaa FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London.

Makubaliano ya mkufunzi Jose Mourinho kuwa kocha wa klabu ya Man United msimu ujao yameafikiwa baada ya mazungumzo ya siku tatu.
Majadiliano kati ya ajenti wa Mourinho Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United yamekamilika ijapokuwa hakuna kandarasi iliotiwa saini.
Tangazo rasmi kutoka kwa klabu hiyo linatarajiwa siku ya Ijumaa.
Raia huyo wa Ureno atachukua mahala pake Louis van Gaal,ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu, siku tatu baada ya United kushinda kombe la FA.

Jose Mourinho anatarajiwa kusaini Mkataba wa kujiunga na Manchester United Ijumaa licha ya kwamba mazungumzo ya pande hizo mbili yanaweza kwisha leo hii.
Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes yupo kwenye mazungumzo na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, Ed Wooward, ambayo yamechukua muda kutokana na utata wa Umiliki wa Haki za Matangazo na Picha kwa upande wa Mourinho.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na Sky Sports, mazungumzo hayo yamepiga hatua na kupata muafaka kwenye ishu nyingi zilizokuwa zikikwamisha na zilizobaki zinatarajiwa kumalizika hii Leo.
Kila upande sasa unategemea Mkataba rasmi utasainiwa Ijumaa.

Hii Leo mambo ya jambo ambalo limemalizwa ni ile ishu ya Jina la Jose Mourinho mwenyewe kumilikiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea kwa kuuzia bidhaa zao kadhaa
Mwenyewe Mourinho inasemekana amehimiza mazungumzo hayo yaishe haraka huku yeye mwenyewe akiwa tayari ashaafiki kuhusu Mshahara na Maslahi yake binafsi ili aanze haraka kazi ya kuijenga upya Man United.
JOSE ameshasaini Mkataba wa kuwa Meneja mpya wa Manchester United.
Man United itamtangaza rasmi Ijumaa baada kuliarifu rasmi Soko la Hisa la New York ambako imesajiliwa kama Kanuni za Makampuni yaliyosajiliwa huko yanavyopasa kufanya.
Mazungumzo kati ya upande wa Mourinho ukiongozwa na Wakala wake Jorge Mendes na Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward yalichukua Siku 3 Jijini London na kukamilika Leo kwenye Saa 11 Jioni kwa majira ya London ambayo ni Saa 1 Usiku kwa Saa za Tanzania.

Mourinho amekuwa hana kibarua tangu Desemba alipoondoka Chelsea na anambadili Louis van Gaal alietimuliwa Jumatatu iliyopita ikiwa ni Siku mbili tu baada ya kuiongoza Man United kutwaa FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London.
Inatarajiwa Mourinho atatua Old Trafford akiwa na Msaidizi wake wa muda mrefu Rui Faria ambae amekuwa nae kila anapokwenda kuanzia huko FC Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid.

Lakini pia zipo habari kwamba Meneja Msaidizi wa Man United Ryan Giggs atabakia Old Trafford na Mourinho mwenyewe ameridhia kuwa nae.

MOURINHO – WASIFU:
Jina kamili: José Mário dos Santos Mourinho Félix
Tarehe ya Kuzaliwa: 26 Januari 1963 (Miaka 53)
Mahali pa kuzaliwa: Setúbal, Portugal

Klabu alizoongoza kama Meneja:
-2000 Benfica
-2001–2002 União de Leiria
-2002–2004 FC Porto
-2004–2007 Chelsea
-2008–2010 Inter Milan
-2010–2013 Real Madrid
-2013–2015 Chelsea

Mataji aliyotwaa:

FC Porto
-Primeira Liga: 2002–03, 2003–04
-Taça de Portugal: 2002–03
-Supertaça Cândido de Oliveira: 2003
-UEFA Champions League: 2003–04
-UEFA Cup: 2002–03

Chelsea
-Premier League: 2004–05, 2005–06, 2014–15
-FA Cup: 2006–07
-Football League Cup: 2004–05, 2006–07, 2014–15
-FA Community Shield: 2005

Inter Milan
-Serie A: 2008–09, 2009–10
-Coppa Italia: 2009–10
-Supercoppa Italiana: 2008
-UEFA Champions League: 2009–10

Real Madrid

-La Liga: 2011–12
-Copa del Rey: 2010–11
-Supercopa de España: 2012