Wednesday, May 25, 2016

JOSE MOURINHO KUMSOGEZA ZLATAN IBRAHIMOVIC MANCHESTER UNITED HIVI KARIBUNI!

SUPASTAA wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ameripotiwa kuwa ameaafikiana na Manchester United kujiunga nao kwa Mkataba wa Mwaka mmoja na huenda akawa ndie Mchezaji wa kwanza kabisa kusainiwa na Jose Mourinho ambae anategemewa wakati wowote ule kuanzia sasa kutangazwa ndie Meneja mpya.

Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, anategemewa kusaini Mkataba huo wa Mwaka mmoja wenye kipengele cha nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi akiwa Mchezaji Huru baada ya Mkataba wake na Paris Saint-Germain.

Msimu huu huko France, Ibrahimovic aliipigia PSG Bao 38 na kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa Taji la Ubingwa kwa mara ya 4 mfululizo.
Mourinho anategemewa kumrithi Louis van Gaal alieondolewa Jana na hilo linaonekana ndilo limemshawishi Ibrahimovic kujiunga na Man united.

Mourinho na Ibrahimovic walikuwa pamoja huko San Siro wakati Inter Milan inapata mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kutwaa Trebo ikiwemo UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2010 wakiifanya inter kuwa Klabu ya kwanza huko Italy kutimiza hilo.

Wawili hao wamekuwa na uhusiano mzuri mno kiasi cha Ibrahimovic kuandika kwenye Kitabu cha Maisha yake kwamba: “Mourinho anaweza kuwa Mtu ninaeweza kuwa tayari kufa kwa ajili yake!”

Mourinho and  Ibrahimovic chat during a training session while the pair were at Inter Milan together
KUHUSU REKODI YA ZLATAN IBRAHIMOVIC
Malmo: 47 appearances, 18 goals
Ajax: 110 apps, 48 goals
Juventus: 92 apps, 26 goals
Inter Milan: 117 apps, 66 goals
Barcelona: 46 apps, 22 goals
AC Milan: 85 apps, 56 goals
PSG: 180 apps, 156 goals