Friday, May 20, 2016

JUMAMOSI ULAYA VIWANJA KUWAKA MOTO FAINALI ZA MAKOMBE-FA CUP SEHEMU MBALIMBALI, COPPA ITALIA, DFB POKAL, COUPE DE FRANCE!

JUMAMOSI Mei 21, Viwanja mbalimbali huko Ulaya vitawaka moto kwa Mechi mbalimbali za Fainali za kugombea Makombe ya Nchi ambayo ni kawaida ndio hufunga rasmi Msimu wa Soka wa Klabu huko Ulaya.  
Kiklabu, huko Ulaya, Msimu wa Soka hufungwa kwa Fainali ya Ubingwa wa Klabu ya kugombea UEFA CHAMPIONS LIGI na safari hii Fainali hiyo itachezwa huko Italy Uwanja wa San Siro Jijini Italy kati ya Klabu za Spain Real Madrid na Mahasimu wao Atletico Madrid ambazo si Mabingwa huko kwao baada ya Ubingwa wa La Liga kubebwa na FC Barcelona huku Real wakimaliza Nafasi ya 3 na Atletico Nafasi ya 4.
Mechi ya kwanza ya Fainali ya Makombe ya Nchi hapo Kesho Jumamosi itakuwepo kule Wembley Jijini London kugombea FA CUP, Kombe kongwe kabisa Duniani kati ya Crystal Palace na Manchester United.
Timu hizo mbili si Mabingwa wa England kwani Ubingwa huo umenyakuliwa na Leicester City.
Fainali nyingine ipo kule Germany Mjini Berlin Uwanja wa Olympiastadion kugombea DFB Pokal kati ya Mabingwa wa Germany Bayern Munich na Borussia Dortmund.

Huko Italy, Fainali ya Coppa Italia itachezwa Stadio Olimpico Mjini Rome kati ya Mabingwa wa Italy Juventus na AC Milan.

Nako huko Stade de France Mjini Paris, Kombe la France litakuwa Uwanjani kugombewa na Mabingwa wa France Paris Saint-Germain.
Kawaida, Washindi wa Makombe haya ikiwa hawana Nafasi za kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI hucheza kwenye UEFA EUROPA LIGI Msimu ujao.

Jumamosi Mei 21
Coppa Italia

21:45 AC Milan v Juventus FC [Stadio Olimpico]
DFB Pokal
21:00 Bayern Munich v BV Borussia Dortmund [Olympiastadion]

FA Cup
19:30 Crystal Palace FC v Manchester United Final [Wembley Stadium]
Coupe de France
22:00 Olympique de Marseille v Paris Saint-Germain [Stade de France]