Sunday, May 22, 2016

JUVE YABEBA COPPA ITALIA

ALVARO MORATA alitoka Benchi na kuipa Juventus Kombe lao la pili mfululizo la Coppa Italia walipowafunga AC Milan 1-0 kwenye Fainali iliyochezwa Jana Uwanja wa Olimpiki Jijini Rome katika Dakika za Nyongeza 30.
Bao hilo la Morata alieingia Uwanjani Dakika ya 108 lilifungwa Dakika ya 110.
Juve sasa wametwaa Mataji Mawili makubwa baada ya pua kuutetea vyema Ubingwa wao wa Serie A.
Hii ni Dabo ya Pili mfululizo kwa Juve lakini pia imewakatili Vigogo AC Milan kucheza Ulaya na badala yake Timu ndogo Sasssuolo kufuzu kucheza EUROPA LIGI kwa mara ya kwanza.

VIKOSI:
AC MILAN:
Donnarumma; Calabria, Zapata, Romagnoli, De Sciglio; Kucka, Montolivo (Jose Mauri 108), Poli (Niang 84); Honda, Bacca, Bonaventura
JUVENTUS: Neto; Rugani, Barzagli, Chiellini; Lichtsteiner (Cuadrado 75), Lemina, Hernanes (Morata 108), Pogba, Evra (Alex Sandro 61); Mandzukic, Dybala