Wednesday, May 11, 2016

KIPA MKONGWE BUFFON KUBAKI JUVE HADI 2018 PAMOJA NA BEKI BARZAGLI

MABINGWA wa Italy Juventus wametangaza kuwa Kipa wao mkongwe Gianluigi Buffon amesaini nyongeza ya Mkataba ambayo itambakisha Klabuni hapo hadi 2018.
Buffon, ambae alitimiza Umri wa Miaka 38 Mwezi Januari, alisaini kuichezea Juve kwa mara ya kwanza 2001 kwa Dau la Rekodi ya Dunia kwa Kipa akitokea Parma na ameshaichezea Juve karibu mara 600 na kutwaa Ubingwa mara 7.
Pia ameichezea Timu ya Taifa ya Italy mara 152 na kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2006.
Sambamba na kumsaini tena Buffon ambae anasifika kuwa mmoja wa Makipa Bora Duniani, Juve pia imefanikiwa tena Sentahafu wao Veterani Andrea Barzagli ambae nae atakuwa hapo Juve hadi 2018 kama Buffon.
Barzagli alijiunga na Juve Mwaka 2011 akitokea Wolfsburg ya Germany
Kufanikiwa kuwafunga tena Wakongwe hao Wawili kumemfanya Rais wa Juve, Andrea Agnelli, ajivune na kusema: “Kuwa na Buffon Kikosini ni heshima na fahari kubwa. Ni Mtu muhimu uWanjani nan je ya Uwanja. Barzagli ni mmoja wa Wachezaji bora tuliowahi kuwasaini. Ni Beki mzuri mno!”