Monday, May 23, 2016

KIRAFIKI: ENGLAND 2 v 1 TURKEY, KANE & VARDY WAIPA USHINDI ENGLAND

ENGLAND wameanza matayarisho yao ya Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, kwa kuishinda 2-1 Turkey katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Etihad Jijini Manchester kwa Bao za Wafungaji Bora wa Ligi Kuu England Harry Kane wa Tottenham na Jamie Vardy wa Mabingwa Leicester City. England walifunga Bao lao Dakika ya 3 kupitia Harry Kane na Turkey kusawazisha Dakika ya 13 kwa Bao la Hakan Calhanoglu.
Kipindi cha Pili Dakika ya 71 England walipata Penati baada ya Jamie Vardy kuangushwa na Topal lakini Harry Kane alikosa Penati hiyo kwa kupiga nje.
Dakika ya 83 Jamie Vardy aliipa England Bao lao la pili kufuatia Kona ambapo Gary Cahill alipiga Kichwa Golini na Kipa wa Turkey Babacan kugongana na Beki wake na kutoa mwanya kwa Vardy kufunga. VIKOSI:
England:
Hart, Walker, Stones, Cahill, Rose, Dier, Wilshere, Alli, Sterling, Kane, Vardy
Akiba: Forster, Bertrand, Henderson, Drinkwater, Barkley, Townsend, Delph, Heaton.
Turkey:
Babacan, Gonul, Balta, Topal, Erkin, Ozyakup, Inan, Tufan, Sen, Calhanoglu, Tosun
Akiba: Kivrak, Ozbayrakli, Yilmaz Calik, Potuk, Sahan, Tore, Koybasi, Malli, Erdinc, Tekdemir, Oztekin, Soyuncu, Mor, Tekin.
REFA: Deniz Aytekin (Germany)

ENGLAND
Ratiba:
Mei 2016
Kirafiki
Ijumaa Mei 27

21:45 England v Australia
Juni 2016
Alhamisi Juni 2
21:45 England v Portugal

EURO 2016 Kundi B
Jumamosi Juni 11

22:00 England v Russia

Alhamisi Juni 16
16:00 England v Wales

Jumatatu Juni 20
22:00 Slovakia v England
Jamie Vardy akishangilia bao lake