Sunday, May 8, 2016

FULL TIME: MANCHESTER CITY 2 v 2 ARSENAL, HAKUNA MBABE! CITY WAWAFUNGULIA MLANGO MAN UNITED SASA!

Alexis Alejandro Sánchez Sánchez  aliisawazishia bao City na kufanya 2-2 dakika ya 68.
Matumaini ya Manchester City ya kumaliza ndani ya 4 bora ya BPL, Ligi Kuu England yamepata msukosuko mkubwa baada ya kubanwa na Arsenal Uwanjani Etihad na kutoka Sare 2-2.
City ndio waliotangulia kwa Bao la Dakika ya 8 la Sergio Aguero ambae alifunga kwa Shuti la chini lakini Arsenal walisawazisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Kichwa la Olivier Giroud kufuatia Kona.
Hadi Mapumziko Bo zilikuwa 1-1.
Kevin De Bruyne akawapa City Bao la Pili kwa juhudi binafsi za kuwahadaa lundo la Mabeki wa Arsenal na kuachia Shuti la chini ambalo lilitinga wavuni Dakika ya 51.
Dakika ya 68 Arsenal walishambulia vizuri na Giroud kumgongea vizuri Alexis Sanchez aliisawazishia Arsenal na Gemu kuwa 2-2 matokeo ambayo yalibaki hadi mwisho.
Matokeo haya yamewachimbia Arsenal kwenye Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 68 lakini City ambao wana Pointi 65 wapo hatarini kuondolewa toka Nafasi ya 4 ikiwa Man United watashinda Mechi yao ya mkononi ya Ugenini na West Ham hapo Jumanne Usiku.


Sergio Leonel Agüero del Castillo dakika ya 8 aliwapachia bao Man City nao Arsenal dakika ya 10 walisawazishiwa bao kupitia kwa mchezaji wake machachari Olivier Giroud. 

Kevin De Bruyne  Kipindi cha pili dakika ya 51 aliwapachikia City bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Arsenal.

Alexis Alejandro Sánchez Sánchez  aliisawazishia bao na kufanya 2-2 dakika ya 68.