Wednesday, May 25, 2016

LIVERPOOL YAMSAINI KIPA LORIS KARIUS TOKA BUNDESLIGA KWA MKATABA WA MIAKA 5


Liverpool waethibitisha dili ya Pauni Milioni 4.7 ya kumsaini Kipa Loris Karius kutoka Klabu ya Bundesliga Mainz ya Germany.
Karius, mwenye Miaka 22, ni Kipa wa Timu ya Taifa ya Germany ya Vijana chini ya Miaka 21.
Kipa huyo Jana alikamilisha upimwaji afya yake na ataanza rasmi Mkataba wake wa Miaka Mitano hapo Julai 1.

Akiichezea Mainz Msimu uliopita, Karius aliweza kukaa Golini na kutofungwa Bao katika Mechi 9 kati ya 34 za Bundesliga wakati Mainz ikimaliza Nafasi ya 6 katika Msimamo wa Ligi hiyo kuu ya Germany.
Akiongea baada ya Dili hii, Karius amesema: “Niliongea na Meneja Jurgen Klopp na nikijasikia vizuri baada ya kuniambia nini anataka kufanya kwa Klabu na Wachezaji wake.”

Karius, ambae aliwahi kuichezea Timu ya Vijana ya Manchester City, ataleta ushindani mkubwa kwa Kipa wa sasa Liverpool ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium, Simon Mignolet, mwenye Miaka 28, ambae Mwezi Januari alisaini Mkataba mpya wa Miaka Mitano.