Monday, May 23, 2016

LOUS VAN GAAL AFUNGASHIWA VIRAGO VYAKE OLD TRAFFORD!

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

Louis van Gaal Ametimuliwa na Klabu ya Man United leo siku mbili baada ya kunyakuwa Kombe la  FA
Van Gaal alipigwa picha akiwa kwenye Gari huko  Aon Training Complex leo Jumatatu asubuhi ambapo leo hii hii kafukuzwa kazi.

Employment lawyer Paul Gilroy QC akiwasili kwenye Maeneo ya  Carrington kumalizia swala la  Van Gaal kuondoka Old Trafford.

Van Gaal akiwa kabeba Mwali wa Kombe la FA Cup Juzi jumamosi

Kocha wa Makipa Frans Hoek (kushoto na Albert Stuivenberg (kulia) nao wametimliwa pamoja na Van Gaal, Huku Ryan Giggs (wa pili kushoto) akisalia kwenye Klabu

Picha ya Pamoja na Van Gaal

Jose Mourinho (anatarajiwa kushika wadhifa wa Van Gaal kwenye Klabu ya Man United)

Mourinho