Tuesday, May 3, 2016

DE GEA NI BORA 2016, SMALLING, MARTIAL, CAMERON, RASHFORD NAO WAZOA TUZO!


KIPA wa Manchester United David de Gea ameweka Historia ya kuwa Mchezaji wa kwanza Klabuni hapo kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka mara 3 mfululizo baada ya Jana kutunukiwa ile ya Mwaka 2016. Kwenye Hafla maalum ya kutunuku Tuzo za Man United iliyofanyika Jana Usiku, De Gea alipewa Tuzo ya Sir Bobby Charlton huku Wachezaji wengine kadhaa wakizoa Tuzo mbalimbali.

“It’s been a bit crazy, it’s difficult to take in.
“It worked in my favour because I wasn’t thinking about the game too much, so I didn’t have to think about it.
“It means a lot. I’m Manchester born. It’s what dreams are made of.
“It’s important I have to thank all my coaching staff, Nicky Butt, Warren Joyce, and my family.”


TUZO ZA MAN UNITED 2016:
-MCHEZAJI BORA: David De Gea
-MCHEZAJI BORA KWA WACHEZAJI: Chris Smalling
-GOLI BORA: Anthony Martial (Kwa Goli lake la kwanza kabisa aliloifungia Man United ikiifunga Liverpool Old Trafford)
-MCHEZAJI BORA U21: Cameron Borthwick-Jackson
-MCHEZAJI BORA U18: Marcus Rashford

Wakati wa Hafla hiyo, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amedai yeye ni mmoja wa 'Mameneja Bora Duniani.'
Pia Van Gaal aliwaponda Wanahabari kwa kumsakama na kuhoji kuhusu kibarua chake kila wakati.
Van Gaal alieleza: "Kwa kuandika kwa Miezi 6 mfululizo kuwa nimefukuzwa mie naweza kuhimili lakini ni ngumu kwa Wachezaji wangu!"
Aliongeza: "Mie sipo kama Wanahabari wanavyochukulia, mimi nina kiburi kwani ni mmoja wa Mameneja Bora Duniani!"