Tuesday, May 17, 2016

MANCHESTER UNITED WAMTUPIA JICHO ZLATAN IBRAHIMOVIC, LIVERPOOL NAO WATAKA KIPA MPYA LORIS KARIUS.


Kipa huyo Mhispania amechoka kufundishwa na Van Gaal na anataka kushinikiza uhamisho kutimkia Real Madrid majira ya joto iwapo Mdachi huyo atabaki Old Trafford
David De Gea ataondoka Manchester United majira ya joto iwapo Louis van Gaal ataendelea kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mujibu wa Daily Mail.

Mhispania huyo ambaye ni mchezaji wa mwaka wa mashabiki kwa msimu wa 2015-16, hajafurahia maisha chini ya Mdachi huyo na atakuwa tayari kulazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid.

 De Gea alikuwa ameshakamilisha kila kitu kutimkia Real Madrid msimu uliopota lakini mambo yakaharibika dakika ya mwisho kutokana na mkanganyiko wa nyaraka.