Thursday, May 5, 2016

MENEJA WA LEICESTER CITY AWATAKA NYOTA WAKE KUTOONDOKA MSIMU HUU


Meneja wa klabu ya Leicester Claudio Ranieri amewataka nyota wake katika kikosi chake kusalia katika timu hiyo kwa mwaka mmoja zaidi. Mbweha hao waliwashangaza wengi kwa kushinda ligi hiyo baada ya kutumia pauni milioni 57 pekee msimu huu.
Winga Riyad Mahrez ,mshambuliaji Jamie Vardy na kiungo wa kati N'golo Kante ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo wanaotarajiwa kuondoka na kujiunga na timu nyengine msimu ujao.
''Nina matumaini tele'',alisema Ranieri.''Musiende''.
'Mkienda timu nyingine huenda msishirikishwe katika mechi''.
Waandishi wa habari walimpatia heshima kwa kusimama kocha huyo wa Italia aliyechukua nafasi ya Nigel Pearson msimu uliopita wakati alipowasili kwenye mkutano na vyombo vya habari.