Thursday, May 12, 2016

MKWANJA BORA DUNIANI: RONALDO ANAONGOZA YUPO JUU, LIONEL MESSI WA PILI, ROONEY WA 6.

KWA mujibu wa Jarida kabambe la Biashara la huko Marekani, Forbes, Cristiano Ronaldo ndie Mchezaji wa Soka anaepata Malipo ya juu kupita yeyote Duniani.
Ronaldo, ambae huichezea Real Madrid ya Spain, alivuna Dola Milioni 82 kwa Mwaka uliopita zikiwa Dola Milioni 53 kama Mshahara na Dola Milioni 29 Mapato yatokanoyo na Matangazo na Udhamini.
Forbes pia limethibitisha kuwa hivi sasa Ronaldo ndie Mwanamichezo anaelipwa vizuri kupita mwingine yeyote katika Michezo yote.
Anaemfuata Ronaldo ni Staa wa Barcelona Lionel Messi alievuna Dola Milioni 77 zikiwa Mshahara ni Dola Milioni 51 na Matangazo na Udhamini Dola Milioni 26.

Kwenye Listi hiyo ya Wachezaji wanaolipwa Mapato ya juu Kepteni wa Manchester United na England, Wayne Rooney, anakamata Nafasi ya 6 akiwa ndie wa kwanza wale Wachezaji wachezao Ligi England akivuna Jumla ya Dola Milioni 26.