Friday, May 6, 2016

MOUSA DEMBELE AFUNGIWA MECHI 6 NA FA

KIUNGO wa Tottenham Mousa Dembele amefungiwa Mechi 6 na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la kufanya vurugu kupindukia.
Dembele alidaiwa kumtia Kidole machoni Straika wa Chelsea Diego Costa wakati wa Mechi ya Chelsea na Spurs Jumatatu Usiku ya Ligi Kuu England Uwanjani Stamford Bridge iliyoisha 2-2 na kuua matumaini ya Spurs kuwa Bingwa na Ubingwa huo kuchukuliwa na Leicester City.
Taarifa ya FA imesema Dembele atatumikia Kifungo chake cha Mechi 6 mara moja ikimaanisha atazikosa Mechi 2 za Spurs zilizobakia Msimu huu pamoja na 4 za kwanza za Msimu upya utakaoanza Agosti.