Sunday, May 8, 2016

NE-YO KUTUA NCHINI MWEZI HUU, KUWASHA MOTO TAMASHA LA JEMBEKA NA VODACOM JIJINI MWANZA.

Ni wakati mwingine tena Vodacom Tanzania inawaletea burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla,Ili waweze kufurahia kwa pamoja kwa kufanikisha hili sasa Vodacom Tanzania,Kushirikiana na Jembe Media Limited tumeamua kumleta mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani NE-YO ambaye ataingia hapa nchini mnamo mwezi huu tarehe 19.NE-YO atawasili nchini kwa ajili ya kutoa burudani ya aina yake katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom 2016 chini ya udhamini mkuu wa Vodacom Tanzania