Tuesday, May 24, 2016

PHIRI AINGIA MSITUNI KUSAKA VIPAJI VIPYA!

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SIKU chache baada ya pazia la ligi kuu ya soka Tanzania bara kufungwa, Kocha mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri ameanza zoezi maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha moja kwa moja kwenye vikosi vya timu yake msimu ujao.

Akizungumza baada ya majaribio ya siku ya kwanza kwa wachezaji wapya vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha vipaji walivyonavyo navyo, Afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa muitikio umekuwa mzuri