Saturday, May 21, 2016

FA CUP FINAL..CRYSTAL PALACE 1 v 2 MANCHESTER UNITED, WEMBLEY STADIUM, JESSE LINGARD AIPA UNITED KOMBE LA FA KWA MARA YA 11


MANCHESTER UNITED wametwaa FA CUP kwa mara ya kwanza tangu 2004 baada ya Jesse Lingard kufunga Bao la ushindi katika Dakika za Nyongeza 30 huku wakiwa Mtu 10 walipoifunga Crystal Palace 2-1 Uwanjani Wembley Jijini London.
Palace walitangulia kufunga Dakika ya 79 kwa Bao la Jason Puncheon lakini Sekunde 175 baadae Kepteni Wayne Rooney aliichambua Palace na kumimina Krosi ambayo Fellaini aliemshushia Juan Mata aliefunga.

Hadi Dakika 90 Bao zilibaki 1-1 na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30.
Kwenye Dakika ya 105 Chris Smalling alipewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 110, Jesse Lingard alieingizwa Dakika ya 90 kumbadili Juan Mata alifunga Bao la ushindi baada ya kazi nzuri ya Rooney.


-Hii ni Mechi ya Fainali ya 135 ya FA CUP.
-Fainali hii ni kama Marudio ya Fainali ya Mwaka 1990 ambayo Manchester United waliifunga Crystal Palace 1-0 baada ya Mechi ya kwanza kwisha Sare 3-3.
-Hii ni mara ya Pili kwa Palace kutinga Fainali wakati kwa Man United ni Fainali ya 18 na wameshinda 11 kati ya hizo wakipitwa tu na Arsenal walioshinda Fainali 12
-Mara ya mwisho kwa Man United kutwaa FA CUP ni Mwaka 2004 walipoifunga Timu ya Daraja la Kwanza Millwall 3-0.

Hili ni Taji la kwanza kwa Meneja Van Gaal kutwaa Taji lake la kwanza akiwa na Man United na pia kuipa Klabu hiyo Kombe la kwanza tangu Sir Alex Ferguson astaafu Mei 2013 ingawa mwanzoni mwa Msimu wa 2013/14, wakiwa chini ya David Moyes, walibeba Ngao ya Jamii walipoibwaga Man City.
Jason Puncheon dakika ya 78 anaipa bao la kuongoza Crystal Palace, Juan Mata dakika ya 81aliisawazishia bao Man United na kufanya 1-1. Dakika 90 zilitimia na kuongezwa dakika 30 huku Manchester United wakicheza pungufu 10 Uwanjani baada Beki wake Chris Smalling kutolewa kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano kuondoshwa kwa kadi nyekundu dakika ya 105, Hapo ndipo Man United walionekana kuzidiwa kwa pengo hilo. Dakika ya 21 kipindi cha nyongeza 30 United walipata bao la ushindi lililofungwa na Jesse Lingard Kipa De Gea akishangiliaSmalling akisepa uwanjani kwa kadi nyekundu aliyooneshwa!Alan Pardew shows off his dance moves in touchline jig to celebrate Jason Puncheon's FAMapumziko sasa bado ni 0-0
Sir Alex Ferguson sakiteta jambo na Mwamuzi Mark Clattenburg kabla ya kipute kuanza

Jake Humphrey, Ian Wright na Rio Ferdinand kablaya Mechi kuanza
VIKOSI:
Manchester United  XI:
De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Mata, Fellaini, Rooney, Martial, Rashford
Man Utd subs: Jones, Young, Romero, Ander Herrera, Schneiderlin, Lingard, Darmian
Crystal Palace starting XI: Hennessey, Ward, Dann, Delaney, Souare, Jedinak, Cabaye, Zaha, McArthur, Bolasie, Wickham
Crystal Palace subs: Speroni, Mariappa, Gayle, Adebayor, Sako, Kelly, Puncheon