Sunday, May 15, 2016

RATIBA: LIGI KUU ENGLAND LEO VIWANJA 10 KUWAKA MOTO, MANCHESTER CITY AU MANCHESTER UNITED KWENYE PATASHIKA KUGOMBEA NAFASI YA 4 KUCHEZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Ligi Kuu England, Leo inafika tamati huku Bingwa na Timu 3 za kushuka Daraja zikiwa zimeshapatika na kilichobaki ni kukaza Nafasi ya 4 Bora ili kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI na UEFA EUROPA LIGI.
Mabingwa wa Msimu huu ni Leicester City wenye Pointi 80 wakifuata Tottenham wenye Pointi 70, Arsenal 68, Man City 65 na Man United 63.
Tayari Leicester, Tottenham na Arsenal zina hakika kucheza UCL na kuacha nafasi ya mwisho kugombewa na City na Mahasimu wao Man United.

City, ambao Leo wapo Ugenini kucheza na Swansea City, wanahitaji Sare tu ili kuinasa Nafasi ya 4 kwani wao wana ubora wa Magoli.
Nafasi za 5 hadi 7 zitazifanya Timu ziende UEFA EUROPA LIGI lakini hili litategemea pia Timu za Man United na Liverpool kwenye Fainali zao za FA CUP na EUROPA LIGI.
Man United watacheza Fainali ya FA CUP na Crystal Palace na Mshindi kwenda EUROPA LIGI wakati Liverpool yupo Fainali ya EUROPA LIGI akiwavaa Mabingwa Watetezi Sevilla huku Mshindi wa Kombe hili akiingizwa UCL.

Mkiani tayari Timu 3 za kushuka Daraja zimepatikana ambazo ni Aston Villa, Norwich City na Newcastle.
Timu zitakazoibadili 3 hizo ni zile zinazopanda Daraja kutoka Championship ambapo 2 zishajulikana na nazo ni Mabingwa wa Chapionship Burnley na Timu ya Pili Middlesbrough wakati Timu ya 3 itapatikan toka Mechi za Mchujo.

RATIBA
Jumapili Mei 15

Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal vs Aston Villa
Chelsea vs Leicester
Everton vs Norwich
Man United vs Bournemouth
Newcastle vs Tottenham
Southampton vs Crystal Palace
Stoke vs West Ham
Swansea vs Man City
Watford vs Sunderland
West Brom vs Liverpool