Thursday, May 5, 2016

STEWART HALL KUITEMA AZAM FC

Wakati kocha huyo ametangaza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu mchana wa leo Shirikisho la soka Tanzania TFF, limetangaza kuipokonya pointi tatu timu hiyo
Kocha wa kikosi cha Azam FC, Muingereza Stewart Hall, amesema ataachana na timu hiyo baada ya ligi kumalizika na hiyo inatokana na matokeo mabaya inayoyapata timu hiyo siku za karibuni.

Hall ameiambia Goal tayari ameuarifu uongozi wa Azam , kuhusiana na mpango wake wa kuondoka Chamazi Complex baada ya kushindwa kupata mafanikio tangu aliporejea kwa mara ya tatu kwenye klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

Katika kipindi cha miezi 13, alichoiongoza Azam Hall, ameweza kushinda taji moja la Kombe la Kagame Julai 2015, lakini alishindwa kukiongoza kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi ya Vodacom na michuano ya Kombe la Shirikisho ambalo walitolewa raundi ya pili na Esperance ya Tunisia.

Wakati kocha huyo ametangaza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu mchana wa leo Shirikisho la soka Tanzania TFF, limetangaza kuipokonya pointi tatu timu hiyo kutokana na kumchezesha beki Erasto Nyoni kwenye mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Mbeya City na sasa timu hiyo imeshushwa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 58.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameiambia Goal, Azam walimtumia beki huyo huku wakijua fika ana kadi tatu za njano katika mchezo huo uliopigwa Febuari 20 Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kwa kukatwa pointi hizo, Azam FC sasa inabakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 na kuporomoka kwa nafasi moja hadi ya tatu, na kupoteza kabisa matumaini ya ubingwa baada ya jana kutoka sare ya mabao 2-2 na JKT Ruvu wakiwa nyumbani Chamazi Complex.

Adhabu hiyo niwazi TFF, imeusogeza ubingwa mlangoni kwa Yanga ambayo sasa itahitaji kushinda mchezo mmoja kati ya mitatu waliyo bakiwa nayo ili kutangazwa mabingwa wapya.