Thursday, May 12, 2016

SUNDERLAND WASHANGAZA KUIFUNGA EVERTON 3-0 NA KUJINUSURU KUSHUKA DARAJA! NEWCASTLE NA NORWICH ZIKISHUKA DARAJA!

Sunderland wamejinusuru kushuka Daraja wakiwa na Mechi moja mkononi kwa kuichapa Everton 3-0 Uwanjani kwao Stadium of Light na kuzifanya Newcastle na Norwich City kuungana na Aston Villa kushuka Daraja na kucheza Championship Msimu ujao.
Sunderland walifunga Bao lao la kwanza kwa Frikiki murua ya Patrick Van Aanholt katika Dakika ya 38 na la pili Dakika ya 42 kwa Goli la Lamine Kone alieachia kigongo ndani ya Boksi kufuata kizaazaa cha Kona.
Hadi Mapumziko Sunderland 2 Everton 0.
Sunderland walifunga Bao lao la 3 Dakika ya 55 baada ya Kona ya Khazri kuokolewa na Kipa Robles na kuleta mshikemshike na Lamine Kone kupata mwanya kufunga.
Baada ya Filimbi ya mwisho Uwanja mzima wa Stadium of Light ululipuka kwa furaha na Meneja wa Sunderland, Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, aliongoza Kikosi kizima cha Timu yake kuzunguka Uwanja na kushukuru Mashabiki wao.NORWICH WAMESHUKA DARAJA PAMOJA NA KUWANYUKA WENZAO WATFORD 4-2