Tuesday, May 3, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN MUNICH 2 v 1 ATLETICO MADRID (Agg 2-2) PEP AKWAMA TENA NYUMBANI! ATLETICO MADRID HAOO FINALI!

Torres nae amekosa penati dakika za mwishoni mwa kipindi cha pili, Mtanange huo ulimalizika kwa bao hizo 2-1 na bao la Ugenini kuwalinda Atletico Madrid na kwenda hatua ya Finali.
Dakika ya 74 Lewandowski aliwapachikia kwa kichwa bao la pili Bayern Munich na kufanya 2-1 dhidi ya Atletico Madrid na matokeo ya jumla(Aggregate) yakiwa 2-2.
Dakika ya 54 Griezann aliwachomoka mabeki wa Bayern na kusawazisha bao kwa kufanya 1-1.Xabi Alonso dakika ya 31 aliwapatia bao la kuongoza Bayern Munich baada ya kutokea mpira wa adhabu na Wachezaji wa Atletico kujichanganya na kutengua mpira na kuzama moja kwa moja langoni. Baadae Bayern tena walipata penati lakini mpigaji Thomas Müller wa (FC Bayern München) alikosa mkwaju huo ambao ulipanguliwa vyema na mlinda lango wa Atletico Mechi ilipomalizika wakatakiana safari njema