Thursday, May 12, 2016

UTAJIRI: REAL MADRID NI YA 1, BARCELONA YA 2, MANCHESTER UNITED YA 3.

Real Madrid ndio Klabu Tajiri Duniani ikitamba mbele ya Barcelona na Manchester United kwa mujibu wa Forbes ambao ni Magwiji wa Taaluma ya Fedha Duniani.
Kwa mujibu wa Jarida la Kimarekani la Forbes, Thamani ya Real Madrid ni Dola Bilioni 3.645 na Mapato yao kwa Mwaka ni Dola 694 Milioni wakiizidi kidogo Barcelona.
Klabu 6 za Ligi Kuu England zipo kwenye 10 Bora huku Man United wakiongoza na nyingine ni Arsenal, Manchester City, Chelsea, Liverpool naTottenham.

FORBES – 10 Bora ya Klabu zenye Thamani Duniani $=Dola (£=Pauni):
1. Real Madrid - US$3.645 bn (£2.52billion)
2. Barcelona - $3.549bn (£2.46bn)
3. Manchester United - $3.317bn (£2.3bn)
4. Bayern Munich - $2.678bn (£1.85bn)
5. Arsenal - $2.017bn (£1.4bn)
6. Manchester City - $1.921bn (£1.33bn)
7. Chelsea - $1.661bn (£1.15bn)
8. Liverpool - $1.548bn (£1.07bn)
9. Juventus - $1.299bn (£900m)
10. Tottenham - $1.017bn (£704m)