Friday, May 20, 2016

WAENDESHA PIKIPIKI NAMNA WANAVYOONGOZA KUVUNJA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KUWAKWEPA MITEGO YA KUKAMATWA NA ASKARI MORO.


Mwendesha pikipiki akiendesha chombo hicho huku akiwa hajavaa kofia ngumu (Helment) kichani muda mfupi kabla ya kupinda kona na kurudi alikotoka wakati akiwakwepa askari wa usalama barabarani waliokuwa wakikamata waendesha pikipiki wasiozingatia sheria za usalama barabara eneo la tuta la stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kupitia askari wa kitengo cha usalama barabara wamekuwa wakiendesha operesheni ya kukamata waendesha pikipiki wasiozingatia sheria za usalama wa barabara.

Chini pichani mwendesha pikipiki huyo zikimuonyesha namna alivyofanikiwa kukwepa askari ili asikamatwe na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.

Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani kwa moja ya sheria hizo ikiwemo ya uvaaji kofia ngumu kichwani inaeleza umuhimu wa uvaaji wa kofia ngumu kichwani hutoa kinga madhubuti endapo dereva wa pikipiki na abiria wake wanaweza kupata ajali na kusaidia kichwa kisiweze kupata madhara.
Askari hao wamekuwa wakikamata makosa ya madevera pikipiki ikiwemo dereva asiyekuwa na leseni, kuvaa kofia ngumu dereva na abiria, bima na upakiaji hatarishi yaani abiria zaidi ya mmoja (mishikaki).





CHINI, Dreva pikipiki akiongea na simu ya kiganjani huku chombo hicho kikiwa katika mwendo
Chini mwenyesha pikipiki akiwa amepakia abiria zaidi ya mmoja jambo ambalo ni kosa kisheria lakini baada ya kuona askari walilazimika kugeuza pipikipi katika mazingira hatarishi na kurudi alikotoka.




Endelea chini hapa kwa picha zaidi...



Picha ya chini dereva wa pikipiki naye alivunja sheria za uslama barabara kama inavyoonyesha katika picha na kuhatarisha usalama wa abiria wake na matukio hayo yalikuwa yakifanywa kwa lengo la kukwepa kukamatwa na askari zaidi ya mita 50 hadi 70 kabla ya kufika eneo waliopo askari


Chini dereva wa pikipiki ya magurudumu matatu naye akiwa ni miongoni mwa madereva waliokuwa wakiwakwepa askari, picha zikimuonyesha akigeuza pikipiki hizo na kugeuza alikotoka.







Dereva huyo picha za hapa chini zinamuonyesha kofia ameining'iniza katika pikipiki hiyo na baada ya kuwaona askari aliamua kuipachika kichwani huku chombo hicho kikiwa katika mwendo akiwa amempakia abiria



Baadhi yao walikamatwa kutokana na kutenda makosa hayo na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani




































Dereva wa pikipiki akiwa amepakia abiria huku yeye akiwa amejikinga na kofia ngumu kichwa na kofia nyingine iliyopaswa kuvaliwa na abiria ikiwa inaning'nizwa katika chomo hicho.