Monday, May 23, 2016

WASHINDI WA SHINDANO LA SHINDA MILIONI NA RED GOLD WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO JIJINI DAR.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum), Amewakabidhi zawadi za washindi wa shindano shinda Mamilioni na la Red-Gold la wiki jijini Dar es Salaam leo.
Shindano hilo la 'Shinda milioni na Red Gold' lenye kauli mbiu ya Ladha na Mtonyo lililoanza kushindaniwa wiki iliyopita na kupata washindi wawili wa milioni 1 na wawili wa laki 5 na wengine laki moja.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni inayotengeneza Matunda na mbogamboga M/s Darsh, Darsh Pandit akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi wa wiki wa shindano la Ladha na Mtonyo lililokuwa likijumuisha watumiaji wa bidhaa za Red Gold.

Mkuu wa Masoko na Biashara, Dominicus Ulikaye akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa shindano la Ladha na Mtonyo lililokuwa likishindanisha walaji wa bidhaa za Red- Gold ambapo mshindi anaweza kujishindia shilingi milioni moja mapaka Laki moja kwa kutumia bidhaa hizo.
Kushiriki ni kununua Bidhaa za Red Gold na kutazama kwenye kifuniko namba na kuzituma kutuma kwenda kwenye kampuni husika.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni M/S Darsh Industries Limited inayotoa bidhaa za Red Gold, Badrish Pandit akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la 'Shinda milioni na Red Gold' lililokuwa kikishindanishwa kwa kutumia bidhaa za Red Gold jijini Dar es Salaam.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akizungumza kabla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la'Shinda milioni na Red Gold' jijini Dar es Salaam leo. Shindano hilo lililuwa likishindanishwa kwa kununua bidhaa za Red Gold na kufungua Kizibo kuangalia kama umeshinda kwa kutuma namba zilizo kwenye kizibo hicho.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.


Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akiwakabidhi washindi wa shindano la 'Shinda Milioni na Red Gold' jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum), Viongozi wa Kampuni M/S Darsh Industries Limited wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.