Tuesday, May 17, 2016

WAYNE ROONEY SASA KUWA KIUNGO TIMU YA TAIFA

Wayne Rooney sio tena mshambuliaji namba moja katika timu ya taifa ya Uingereza,amesema nahodha wa zamani wa timu hiyo Alan Shearer.
Rooney ambaye anaongoza rekodi ya ufungaji wa muda wote ametajwa katika kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
Shearer amesema Rooney mwenye miaka 30 anafaa zaidi katika nafasi ya kiungo nyuma ya Harry Kane na Jamie Vardy.
''Lazima pawepo nafasi kwa ajili ya nahodha wa timu na vizuri imekuwepo''alisema.Lakini siku za Wayne kuw mshambuliaji wa kwanza zimeisha. ''Nafikiri Harry Kane na Jamie Vardy wanapaswa kuanza mbele lakini bado Rooney ana nafasi kubwa ya kucheza ama namba kumi ama kiungo wa kati. Rooney ni miongoni mwa washambuliaji watano walioitwa katika kikosi cha Roy Hodson siku ya jumatatu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.Wengine ni Harry Kane,Jamie Vardy, Daniel Sturridge na Marcus Rashford.