Sunday, May 15, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC AIAGA PARIS ST-GERMAIN KWA KUIPA UBINGWA


Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amepachika magoli mawili katika mchezo wake wa mwisho akiwa na Paris St-Germain walioibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Nantes na kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufanrasa.
Nyota huyo wa Paris St-Germain anayeongoza kwa kuifungia magoli mengi timu hiyo anayeondoka kwenye timu hiyo katika majira ya msimu wa joto, alilazimisha mchezo kusimama baada ya dakika kumi wakati mashabiki wa PSG waliposimama na kumpongeza kwa mafanikio.

Kwa kufunga magoli mawili katika mchezo wa jana Ibrahimovic amevunja rekodi nyingine ya klabu hiyo, kwa kuwa mchezaji aliyeifungia PSG magoli mengi katika ligi kwa msimu mmoja ambapo amefunga magoli 38.


Zlatan Ibrahimovic akiwa amenyanyua juu kombe la Ligi Kuu ya Ufaransa baada ya kutawazwa mabingwa

Zlatan Ibrahimovic akiwa amewabeba watoto wawili waliovaa jezi zenye ujumbe maalum kwake