Thursday, June 30, 2016

AC MILAN YAMTEUA MONTELLA KOCHA MKUU MPYA!

AC Milan imemsimika Vincenzo Montella kama Kocha Mkuu wao mpya akimbadili Cristian Brocchi.
Baada ya ripoti kuzagaa sana kuhusu uteuzi wa Montella, AC Milan sasa imethibitisha kuwa Kocha huyo wa Sampdoria sasa atachukua mikoba kuiongoza AC Milan inayotumia Uwanja wa San Siro Jijini Milan.
Rais wa AC Milan, Silvio Berlusconi, pamoja na wanaotarajiwa kuwa Wawekezaji wapya kutoka China, wote wameafiki uteuzi wa Montella.
Montella alianzia kazi ya Ukocha huko AS Roma alipochukua nafasi ya Claudio Ranieri na kuweza kuifikisha Nafasi ya 6 kwenye Serie A Mwaka 2011.

Kisha Montella akahamia Catania na baadae Fiorentina ambako aliweza kuwapa Nafasi ya 4 ya Serie A kwa Misimu Mitatu mfululizo.

Lakini baada ya kukwaruzana na Uongozi, Montella akatimuliwa Fiorentina na kwenda Sampdoria Novemba Mwaka Jana kumbadili Walter Zenga.