Tuesday, June 7, 2016

AFCON 2017: 10 ZIMETINGA FAINALI BADO 6

NCHI 10 tayari zimejipatia nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2017 Mwakani huko Gabon.
Pamoja na Wenyeji Gabon ambao wanaingia Fainali moja kwa moja Nchi ambazo zimefuzu kabla kumaliza Mechi zao za Makundi ni Algeria, Cameroun, Ghana, Mali, Morocco, Senegal na Zimbabwe.
Pia wapo Egypt, ambao ndio wenye Rekodi ta kulibeba Kombe hili mara nyingi wakilitwaa mara 7, na wapo Guinea-Bissau ambao hii ni mara ya kwanza kucheza Fainali za AFCON.
Nafasi 6 zilizobaki za kucheza Fainali ambazo 4 ni za Washindi wa Makundi na 2 ni za Tiketi ya Washindi wa Pili Bora wa Makundi, zitajazwa kwenye za Raundi ya mwisho za Makundi hapo Septemba 2-4.
HALI ILIVYO KUNDI KWA KUNDI:
KUNDI A

Tunisia watakuwa Wenyeji wa Liberia na Mshindi wa Mechi hii atafuzu lakini wakitoka Sare ya 0-0 Togo atapenya ikiwa watawafunga 'vibonde' Djibouti kwenye Mechi ambayo Togo wako kwao.
Sare ya Magoli kati ta Tunisia na Liberia itawafanya Liberia waingie Fainali.
KUNDI B
Congo DR watakuwa Wenyeji wa Central African Republic huku wakiongoza Kundi kwa Pointi 2 mbele na Sare kwao itawaingiza Fainali.
KUNDI C
Mali wana hakika ya kucheza Fainali ama kwa kushinda Kundi au kwa kutwaa moja ya Tiketi 2 za Washindi wa Pili Bora.
Benin watashinda Kundi ikiwa watazifunga Equatorial Guinea Jumapili ijayo na Mali ugenini katika Mechi ya mwisho.
KUNDI D
Burkina Faso na Uganda zitamaliza Mechi zao za Kundi wakiwa makwao na ushindi kwao utazipeleka Fainali kwa mmoja kuwa Mshindi wa Kundi na mwingine kwa Tiketi ya Mshindi wa Pili Bora.
KUNDI E
Guinea- Bissau wapo Fainali.
KUNDI F
Morocco wapo Fainali.
KUNDI G
Egypt wapo Fainali.
KUNDI H
Ghana wapo Fainali
KUNDI I
Mabingwa Watetezi wa Afrika Ivory Coast wanahitaji Sare ya Nyumbani na Sierra Leone ili watinge Fainali.
KUNDI J
Algeria wako Fainali.
KUNDI K
Senegal wapo Fainali.
KUNDI L
Zimbabwe wapo Fainali.
KUNDI M
Cameroun wapo Fainali.