Sunday, June 19, 2016

CAF CC: WAPINZANI WA YANGA KUNDI A, TP MAZEMBE WAITWANGA MEDEAMA HUKO LUBUMBASHI

WAPINZANI wa Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga kwenye Kundi A la Mashindano ya Klabu Barani Afrika ya KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC, TP Mazembe ya Congo DR na Medeama ya Ghana Leo wamepambana huko Stade TP Mazembe Mjini Lubumbashi Nchini Congo DR.
TP Mazembe ilibidi wajitutumue na kutoka nyuma kwa Bao 1 na mwishowe kuichapa Medeama 3-1.
Medeama walitangulia kufunga Bao lao katika Dakika 4 tu kupitia Malik Akowuah na Mazembe kujibu Dakika ya 21 kwa Bao la Rainford Kalaba na kisha kupiga Bao la Pili Dakika ya 45 Mfungaji akiwa Salif Coulibaly na kufunga Bao la 3 Dakika ya 73 kupitia Rainford Kalaba.
Baadae Leo, Saa 6:15 Usiku, kwa Saa za hapa Tanzania, Yanga watajitupa Ugenini huko
Stade Unite Africaine Mjini Bejaia Nchini Algeria kuivaa MO Bejaia katika Mechi nyingine ya Kundi A.

Baada ya Mechi hizi za kwanza za Kundi A, Mechi za Pili ni hapo Juni 28 wakati Yanga watakapoikaribisha TP Mazembe Juni 28 na Siki inayofuata Medeama wako kwao Ghana kucheza na MO Bejaia.


CAF Kombe la Shirikisho:
KUNDI A:

-MO Bejaia (Algeria)
-Yanga (Tanzania)
-TP Mazembe (DR Congo)
-Medeama (Ghana)


KUNDI B:
-KAC Marrakech (Morocco)
-Etoile du Sahel (Tunisia)
-FUS Rabat (Morocco)
-Ahly Tripoli (Libya)


MECHI ZA MAKUNDI
RATIBA/MATOKEO:

Mechi za 1
Ijumaa Juni 17

KAC Marrakech – Morocco 2 ES Sahel – Tunisia 1

Jumapili Juni 19
FUS de Rabat – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya
MO Bejaia – Algeria v Yanga - Tanzania
TP Mazembe - Congo, DR 3 Medeama – Ghana 1


Mechi za 2
Juni 28

Al-Ahli Tripoli – Libya v KAC Marrakech - Morocco
Yanga - Tanzania v TP Mazembe - Congo, DR

Juni 29
ES Sahel – Tunisia v FUS de Rabat - Morocco
Medeama – Ghana v MO Bejaia - Algeria


Mechi za 3
Julai 15

KAC Marrakech – Morocco v FUS de Rabat - Morocco
Yanga - Tanzania v Medeama - Ghana

Julai 16
ES Sahel – Tunisia v Al-Ahli Tripoli - Libya
Julai 17
MO Bejaia – Algeria v TP Mazembe - Congo, DR


Mechi za 4
Julai 26

Al-Ahli Tripoli – Libya v ES Sahel - Tunisia
Medeama – Ghana v Yanga – Tanzania

Julai 27
FUS de Rabat – Morocco v KAC Marrakech - Morocco
TP Mazembe - Congo, DR v MO Bejaia - Algeria


Mechi za 5
Agosti 12
Al-Ahli Tripoli – Libya v FUS de Rabat - Morocco

Agosti 13
ES Sahel – Tunisia v KAC Marrakech - Morocco
Yanga – Tanzania v MO Bejaia – Algeria

Agosti 14
Medeama – Ghana v TP Mazembe - Congo, DR
Mechi za 6
Agosti 23
KAC Marrakech – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya
FUS de Rabat – Morocco v ES Sahel - Tunisia
TP Mazembe - Congo, DR v Yanga - Tanzania
MO Bejaia – Algeria v Medeama - Ghana

NUSU FAINALI
Mechi za Kwanza Septemba 16-18 na Marudiano Septemba 23-25
Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A
Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A


FAINALI
Mechi ya Kwanza Oktoba 28-30 na Marudiano Novemba 4-6