Friday, June 17, 2016

CAF CC: WIKIENDI MAKUNDI KUANZA, YANGA KUTUA MJINI BEJAIA, ALGERIA

WIKIENDI hii Mashindano ya Klabu Barani Afrika ya KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC, yataanza Mechi zake za Makundi.

Yapo Makundi Mawili ya Timu 4 kila moja na Yanga, ambayo ndio Timu pekee ya Tanzania kwenye Mashindano ya Kimataifa, ipo Kundi A pamoja na Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Congo DR na nyingine ni MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.

Yanga, chini ya Kocha kutoka Holland, Hans van Pluijm, Wiki yote hii walikuwa huko Ulaya Nchini Uturuki wakijifua na Leo wanatarajiwa kutua Nchini Algeria kwa ajili ya Mechi yao ya kwanza na MO Bejaia ambayo itachezwa Jumapili Uwanja wa Unit̩ Maghr̩bine РBejaia Mjini Bejaia Nchini Algeria.

Refa wa Mechi hii ni Bouchaib El Ahrach kutoka Morocco.wenye hatua hii, Yanga imeongeza Wachezaji wapya Wanne ambao tayari CAF imesharidhia kuwasajili rasmi.

Wachezaji hao ni Beki Hassan Ramadhan Kessy alietokea Simba, Kiungor Juma Mahadhi kutoka Coastal Union, Beki Vincent Andrew toka Mtibwa Sugar na Kipa Beno Kakolanya aliekuwa Tanzania Prisons.


Kikosi cha Yanga ambacho kimesafiri ni:
Makipa: Ally Mustafa, Deo Munishi, Benno Kakolanya
Mabeki: Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Nadir Haroub, Vincent Bossou.
Viungo: Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya
Mafowadi: Donald Ngoma, Matheo Anthony, Amis Tambwe.
CAF Kombe la Shirikisho:
KUNDI A:
-MO Bejaia (Algeria)
-Yanga (Tanzania)                                                                                    
-TP Mazembe (DR Congo)
-Medeama (Ghana)
KUNDI B:
-KAC Marrakech (Morocco)
-Etoile du Sahel (Tunisia)
-FUS Rabat (Morocco)
-Ahly Tripoli (Libya)
RATIBA
MECHI ZA MAKUNDI
Mechi za 1
Ijumaa Juni 17
KAC Marrakech – Morocco v ES Sahel - Tunisia
Jumapili Juni 19
FUS de Rabat – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya        
MO Bejaia – Algeria v Yanga - Tanzania 
TP Mazembe - Congo, DR v Medeama - Ghana
Mechi za 2
Juni 28
Al-Ahli Tripoli – Libya v KAC Marrakech - Morocco      
Yanga - Tanzania    v TP Mazembe - Congo, DR
Juni 29
ES Sahel – Tunisia v FUS de Rabat - Morocco  
Medeama – Ghana v MO Bejaia - Algeria
Mechi za 3
Julai 15
KAC Marrakech – Morocco v FUS de Rabat - Morocco
Yanga - Tanzania    v Medeama - Ghana
Julai 16
ES Sahel – Tunisia v Al-Ahli Tripoli - Libya
Julai 17
MO Bejaia – Algeria v TP Mazembe - Congo, DR        
Mechi za 4
Julai 26
Al-Ahli Tripoli – Libya v ES Sahel - Tunisia        
Medeama – Ghana v Yanga – Tanzania
Julai 27
FUS de Rabat – Morocco v KAC Marrakech - Morocco
TP Mazembe - Congo, DR v MO Bejaia - Algeria
Mechi za 5
Agosti 12
Al-Ahli Tripoli – Libya v FUS de Rabat - Morocco        
Agosti 13
ES Sahel – Tunisia v KAC Marrakech - Morocco
Yanga – Tanzania v MO Bejaia – Algeria
Agosti 14
Medeama – Ghana v TP Mazembe - Congo, DR
Mechi za 6
Agosti 23
KAC Marrakech – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya      
FUS de Rabat – Morocco v ES Sahel - Tunisia   
TP Mazembe - Congo, DR v Yanga - Tanzania  
MO Bejaia – Algeria v Medeama - Ghana
NUSU FAINALI
**Mechi za Kwanza Septemba 16-18 na Marudiano Septemba 23-25
Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A
Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A
FAINALI
Mechi ya Kwanza Oktoba 28-30 na Marudiano Novemba 4-6