Sunday, June 19, 2016

COPA AMERICA CENTENARIO: NUSU FAINALI JUMATANO WENYEJI USA vs ARGENTINA

COPA AMERICA CENTENARIO inayochezwa huko Marekani sasa imeingia hatua ya Nusu Fainali ambapo Jumatano ni Wenyeji USA kucheza na Argentina na Alhamisi ni Colombia dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Copa America Chile.
Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916.
Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.
Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.
Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.

Kawaida Mshindi wa Copa America huiwakilisha Marekani ya Kusini kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho lakini Mshindi wa Copa América Centenario hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile, wakiwa Nyumbani kwao, ndio walitwaa Copa America ya kawaida na wao ndio watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho Mwakani, 2017, huko Russia.

WAKATI HUO HUO, Straika Chile anaechezea Klabu ya Germany 1899 Hoffenheim, Eduardo Vargas, ndie anaongoza kwenye mbio za Buti ya Dhahabu ya Mashindano haya akiwa na Bao 6 kwa Mechi 4 akifuatiwa na Gwiji wa Argentina Lionel Messi mwenye Bao 4 kwa Mechi 3.

COPA AMERICA
RATIBA
NUSU FAINALI
Jumatano 22 Juni 2016

04:00 USA v Argentina

Alhamisi 23 Juni 2016

03:00 Colombia v Chile

MSHINDI WA TATU
Jumapili 26 Juni 2016

02:00


FAINALI
Jumatatu 27 Juni 2016
03:00