Tuesday, June 7, 2016

DOKTA EVA CARNEIRO AFUTA KESI DHIDI YA MOURINHO NA CHELSEA.

DAKTARI wa zamani wa Timu ya Chelsea Mwanamama Eva Carneiro ameamua kuifuta Kesi yake dhidi ya Klabu ya Chelsea na aliekuwa Meneja wao Jose Mourinho aliyoipeleka Mahakamani akidai kufukuzwa kazi bila kutendewa haki.
Game over: Jose Mourinho grins as he is rushed into a waiting car after he and Chelsea settled with the club's former doctor Eva CarneiroWakati Kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa Mahakamani Mjini London ambako Jumatatu iliibuka hoja kuwa Dokta huyo aliikataa Ofa ya Chelsea ya kumlipa Pauni Milioni 1.2 kama maslahi yake ili pia asiende Mahakamani, Leo hii upande wa Dokta huyo umethibitisha kufikiwa makubaliano ya kumaliza tofauti zao nje ya Mahakama kitu ambacho hata upande wa Chelsea na Mourinho umethibitisha.
Exchange: Dr Carneiro claims that she 'clearly heard' Jose call her a 'daughter of a whore' as she ran onto the pitch in an incident that led to this touchline row, and eventually her exit from the clubHata hivyo, pande zote zimesema nini wamekubaliana kumaliza Kesi hiyo nje ya Mahakamani ni siri ya pande hizo mbili.
Dokta Eva Carneiro-Sakata lilivyoendelea:
8 Agosti 2015: Mourinho amshutumu Carneiro kwa kuwa "mjinga"
22 Septemba: Carneiro anaachana na Chelsea
30 Septemba: Mourinho asafishwa na FA kumshutumu Carneiro
30 Septemba: Uamuzi wa FA kuhusu Mourinho wapingwa na Makundi
1 October: Bosi wa FA Dyke amponda Mourinho 

Dokta Carneiro aliondoka Chelsea Mwezi Septemba baada ya kushushwa cheo na kupigwa marufuku kuihudumia Timu ya Kwanza.

Sakata la Dokta Eva Carneiro na Mourinho liliibuka kwenye Mechi ya Agosti 8 ya Ligi Kuu England waliyotoka 2-2 na Swansea City Uwanjani Stamford Bridge.

Katika Mechi hiyo,Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.

Mourinho alimponda Dokta huyo na kumsema hajui mchezo unakwendaje.