Saturday, June 18, 2016

EURO 2016: BELGIUM YAITWANGA REPUBLIC OF IRELAND BAO 3-0

LEO Belgium imeitwanga Republic of Ireland 3-0 Uwanjani Stade de Bordeaux Mjini Bordeaux Nchini France katika Mechi ya Kundi E la EURO 2016.
Hadi Mapumziko Gemu ilikuwa 0-0.

Kipindi cha Pili Belgium walikuja juu na kufunga Bao zao kupitia Romelu Lukaku baada ya kazi njema ya Kevin De Bruyne kisha Axel Witsel kufunga kwa Kichwa kutoka Krosi ya Meunier na la tatu kupigwa tena na Lukaku baada ya Kepteni Hazard kuchomoka na mpira vizuri na kumpasia.