Friday, June 17, 2016

EURO 2016: CZECH REPUBLIC 2 vs 2 CROATIA

CZECH REPUBLIC Leo wametoka nyuma kwa Bao 2-0 na kupata Sare ya 2-2 walipocheza na Croatia kwenye Mechi ya Kundi D iliyochezwa huko Stade Geoffroy Guichard, St Etienne, France.
Bao za Croatia zilifungwa Dakika za 38 na 59 kupitia Ivan Perisic na Ivan Rakitic wakati za Czech Republic zilifungwa Dakika za 75 na 94 kupitia Milan Skoda na Tomas Necid kwa Penati.
Mechi hii ilisimamishwa kwa Dakika 5 kwenye Dakika ya 85 na Refa kutoka England Mark Clattenburg huku Croatia wakiwa mbele 2-1 baada ya Mashabiki wa Croatia kurusha Fataki Uwanjani zilizoshika Moto.
Mara baada ya Mpira kuanza tena, katika Dakika za Nyongeza, Dakika ya 94, Refa Clattenburg aliwapa Penati Czech Republic baada ya Beki Domagoj Vida kuunawa Mpira na Tomas Necid kufunga kwa Mkwaju mkali.