Friday, June 17, 2016

EURO 2016: ENGLAND 2 v 1 WALES

ENGLAND wametoka nyuma kwa Bao 1 na kuwatwanga Wales 2-1 ndani ya Stade Bollaert-Delelis Mjini Lens Nchini France kwenye Mechi ya Kundi B na kuwapaisha hadi kileleni mwa Kundi hilo huku Mechi ikibaki 1 tu.
Wales, ambao hawajawahi kuifunga England tangu 1984 waliposhinda 1-0 kwa Bao la Mark Hughes, ambae sasa ni Meneja Stoke City, alipocheza Mechi yake ya kwanza kwa Wales, walitangulia kuifunga England kwa Frikiki ya Dakika ya 42 iliyopigwa na Gareth Bale umbali wa Mita 30 na Kipa Joe Hart kufanya makosa.

Baada ya kuona mambo yanaharibika Kocha wa England, Roy Hodgson, aliwatoa Harry Kane na Raheem Sterling katika Dakika ya 45 na kuwaingiza Jamie Vardy na Daniel Sturridge na baadae kumuingiza Chipukizi Marcus Rashford ambae aliweka Rekodi ya kuwa Kijana mdogo kuichezea EURO England.

Jamie Vardy aliisawazishia England Dakika ya 56 na Sturridge kuipa England Bao la ushindi Dakika ya 92.

Ushindi huu umewaweka England kileleni mwa Kundi B wakiwa na Pointi 4 wakifuata Wales na Slovakia wenye Pointi 3 kila mmoja na Russia mkiani wakiwa na Pointi 1 tu.