Thursday, June 23, 2016

EURO 2016: ITALY 0 vs 1 REPUBLIC OF IRELAND

Republic of Ireland hao hatua ya 16 Bora
KUNDI E la EURO 2016 limemaliza Mechi zake kwa Belgium na Republic of Ireland kuungana na Italy waliofuzu kabla kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwenye Mashindano hayo yanayochezwa Nchini France.
Huko Stade Pierre Mauroy Mjini Lille, Republic of Ireland walipata Bao lao pekee na la ushindi kupitia Robbie Brady kwenye Dakika ya 84 dhidi ya Italy iliyobadili Wachezaji 8 toka Kikosi kilichocheza Mechi mbili zilizopita.
Nako huko Stade de Nice, Mjini Nice, Sweden walifungwa Bao pekee Dakika ya 84 kwa mzinga mkali wa Radja Nainggolan na kutupwa nje ya EURO wakimstaafisha Staa wao Zlatan Ibrahimovic kwa huzuni.
Matokeo hayo yamefanya Italy, licha ya kufungwa, wawe Washindi wa Kundi na Belgium kumaliza Nafasi ya Pili wakati Republic of Ireland wakiwa Nafasi ya 3 na kufuzu kama moja ya Timu 4 zilizomaliza Nafasi za Tatu Bora.