Friday, June 17, 2016

EURO 2016: ITALY WAUNGANA NA WENYEJI FRANCE KUSONGA MTOANO, EDER AFANYA MAMBO DAKIKA ZA MAJERUHI!


ITALY wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 1 mkononi baada ya Leo kuichapa Sweden 1-0 huko Stadium de Toulouse Mjini Tolouse, France kwa Bao la Dakika ya 88 katika Mechi ya Kundi E la la EURO 2016.
Bao hilo lilifungwa baada ya Mpira wa kurushwa na Giorgio Chiellini Kuguswa kwa Kichwa na Simone Zaza, alieanzia Benchi, na Éder Eder Citadin Martins na kuwatoka Wachezaji Watatu wa Sweden na kufunga.