Tuesday, June 7, 2016

EURO 2016 KUANZA KUTIMUA VUMBI IJUMAA HII, SHERIA MPYA ZA SOKA KUTUMIKA!

MASHINDANO ya kuwania Ubingwa wa Mataifa ya Ulaya EURO 2016 yanaanza huko France Ijumaa Juni 10 na jipya kubwa ni kuanza kutumika kwa mabadiliko ya Sheria za Soka.

Wabadilishaji na Watungaji Sheria za Soka, IFAB, International Football Association Board, walipitisha mabadiliko hayo mapya, ambayo yapo 95, yaanze kutumika Juni 1 na Wiki moja nyuma Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya England na Turkey iliamua kutumia Sheria hizo mpya ili kujizoeza na hali kabla EURO 2016 haijaanza.
Moja ya mabadiliko hayo ni kufuta ile Adhabu ya Kadi Nyekundu anayopewa Mchezaji akimzuia Mpinzani isivyo halali wakati akienda kufunga.

IFAB:

-Ni International Football Association Board ambayo ina Wajumbe 8: FIFA hutoa Wanne na Nchi za England, Scotland, Northern Ireland na Wales (ambazo ndizo Nchi zonazohesabika kuanzisha mchezo wa Soka), hutoa Wajumbe 4.
Makubwa kwenye Sheria hizi mpya ni urahisi wa Lugha iliyotumika ili kuweka waziwazi utumiaji wa Sheria hizo.

BAADHI YA MABADILIKO YA SHERIA:
Sheria ya 1 – Uwanja wa Kuchezea


-Nembo zitatumika kwenye Vibendera vya Kona [Kabla ilikuwa haziruhusiwi]

-Mchanganyiko wa Uwanja wa Kuchezea Bandia na ule wa Majani halisi ruksa kutumiwa [Kabla ilikuwa haziruhusiwi]

Sheria ya 3 - Wachezaji

-Ikiwa Mchezaji wa Akiba, yule alietolewa kwa Kadi Nyekundu au Mwamuzi ataingilia Mchezo na kusababisha usimame, itapigwa Frikiki ya moja kwa moja au Penati [Kabla ilikuwa inapigwa Frikiki isiyo ya moja kwa moja au Mpira unadondoshwa kati ya Wapinzani Wawili].
-Ikiwa Mchezaji wa Akiba, Afisa wa Timu au Mtu mwingine wa nje atauzuia Mpira kutinga Golini, Refa anaweza kutumia Sheria ya kutoa manufaa na kukubali Goli.

Sheria ya 4 – Vifaa vya Wachezaji
-Mchezaji anaetumia nguo chini ya Bukta yake anatakiwa awe na nguo hiyo yenye rangi sawa na wenzake wa Timu moja waliovaa hivyo hivyo na pia rangi hiyo iwe sawa na Bukta zao.

-Mchezaji anaetoka nje ya Uwanja kubadili Buti ataruhusiwa kurudi tena Uwanjani na Refa.

Sheria ya 5 - Refa
-Refa watakuwa na uwezo wa kuchukua hatua tangu pale wanapokanyaga Uwanjani kwa ajili ya kuukagua kabla ya Mechi kuanza na si mwanzo wa Mchezo. Hii inamaanisha Refa anaweza kumtoa Mchezaji kwa Kadi Nyekundu hata wakati ule akipasha moto kabla Mechi kuanza lakini Kadi za Njano zitatolewa tu baada ya Mechi kuanza.

-Mchezaji akiumizwa na Mpinzani ambae atapewa Kadi Nyekundu halazimiki kutoka nje ya Uwanja kwa matibabu.

Sheria ya 7 – Muda wa Mechi
-Muda utakaotumiwa kwa mapumziko ya kupata vinywaji sasa unaweza ukaongezwa mwishoni mwa Mechi.

Sheria ya 8 – Kuanza na kuanzishwa tena Mchezo
-Si lazima Mpira usogezwa mbele tu wakati wa kuanzisha Gemu, unaweza tu ukapelekwa kokote.

-Refa hapaswi kuamrisha nani aguse mwanzo wakati Mpira unapoanzishwa tena kwa kurushwa juu kati Wapinzani.

Sheria ya 10 – Kuamua Matokeo ya Mechi

-Kuamua Goli lipi litumike kupigia Mikwaju ya Penati Tano Tano itaamuliwa kwa kurusha Sarafu kwa kupima hali ya Uwanja na usalama na si uamuzi wa Refa.

-Timu itakayokuwa na Wachezaji wengi kupita Mpinzani wake wakati Mikwaju ya Penati Tano Tano inaanza watapaswa kupunguza Wachezaji wao wawe idadi sawa na ile yenye Wachezaji pungufu ili wasinufaike na kuwa na Wachezaji wazuri wa Penati.

Sheria ya 11 - Ofsaidi
-Mikono ya Mchezaji haihesabiki katika kuamua Mchezaji ni Ofsaidi.

-Frikiki zinazotokana na uamuzi wa Ofsaidi zinaweza kupigwa tokea pale yule Mchezaji alie Ofsaidi alipopokea Mpira.

Sheria ya 12 – Faulo na Utovu wa Nidhamu
-Frikiki au Penati inaweza tu kutolewa wakati Mpira ukiwa unachezwa.
-Kumzuia Mpinzani kwenda kufunga isivyo halali ndani ya Penati Boksi hakutapaswa kupewa Kadi Nyekundu ya moja kwa moja labda kosa dhidi ya Mpinzani liwe la kumshika, kumvuta au kumsukuma, au kusiwe na jaribio la kucheza Mpira au kukaba, au kosa jingine lolote linalostahili Kadi Nyekundu.

-Kumpiga Mpinzani ni kosa la Kadi Nyekundu popote linapotendeka.

-Kosa dhidi ya Mwamuzi litatolewa Frikiki ya moja kwa moja au Penati.

Sheria ya 13 - Frikiki
-Ikiwa Faulo itafanyika nje ya Uwanja wakati Mpira unachezwa, Mechi itanzishwa tena kwa Frikiki ya moja kwa moja itayopigwa pale kwenye Mstari wa Mpaka wa Uwanja karibu na kosa lilipotendeka. Kwa Faulo hizo, Frikiki ya moja kwa moja itatolewa kwa makossa yanayostahili Frikiki ya moja kwa moja na Penati itatolewa ikiwa Faulo itatendwa mkabala na eneo la Penati.

Sheria ya 14 – Upigwaji Penati
-Wachezaji wanaogushia kupiga Penati wakati washaufikia Mpira wataadhibiwa kwa Kadi ya Njano lakini kugushi wakati unakimbia kwenda pale Mpira ulipowekwa inaruhusiwa. Makipa wanaovuka Mstari wa Goli mapema kabla Penati haijapigwa wataadhibiwa kwa Kadi ya Njano.

Sheria ya 15 – Mpira wa Kurusha
-Wapinzani wanaozuia Mpira wa Kurushwa wakiwa chini ya Mita 2 toka kwa Mrushaji wataonywa.

Sheria ya 17 – Mpira wa Kona
-Sheria hii imebadilishwa na kutamka Mpira utakuwa umepigwa ukiguswa na kusogea nah ii ni kuondoa ule ujanja wa kuugusa tu Mpira na kuhadaa Kona imepigwa ili kunufaika.


EURO 2016 - Fainali
MAKUNDI:

KUNDI A: France, Romania, Albania, Switzerland.
KUNDI B: England, Russia, Wales, Slovakia.
KUNDI C: Germany, Ukraine, Poland, Northern Ireland.
KUNDI D: Spain, Turkey, Czech Republic, Croatia.
KUNDI E: Belgium, Republic of Ireland, Sweden, Italy.
KUNDI F: Portugal, Iceland, Austria, Hungary.

Fainali zitafanyika lini:

-Euro 2016 itaanza Ijumaa Juni 10 na kumalizika Jumapili Julai 10.

-Hii ni mara ya kwanza kwa Fainali hizi kuwa na Timu 24 na hivyo itakuwepo Raundi ya Mtoano ya Timu 16, kisha Robo Fainali na Nusu Fainali.


Viwanja vya Mechi za Fainali:

Euro 2016 itatumia Viwanja 10 Nchini France:
Stade de Bordeaux, Bordeaux (Watu 42,000)
Stade Bollaert Delelis, Lens Agglo (35,000)
Stade Pierre Mauroy, Lille Metropole (50,100)
Stade de Lyon, Lyon (58,000)
Stade Velodrome, Marseilles (67,000)
Stade de Nice, Nice (35,000)
Parc des Princes, Paris (45,000)
Stade de France, Saint-Denis (80,000)
Stade Geoffroy Guichard, Saint-Etienne (41,500)
Stadium de Toulouse, Toulouse (33,000)
 

Fainali itachezwa Stade de France
EURO 2016
Ratiba
Ijumaa Juni 10

KUNDI A, France v Romania (2300, Stade de France, Paris)

Jumamosi Juni 11

KUNDI A, Albania v Switzerland (1700, Stade Bollaert-Delelis, Lens)
KUNDI B, Wales v Slovakia (2000, Stade de Bordeaux)
KUNDI B, England v Russia (2300, Stade Velodrome, Marseille)

Jumapili Juni 12

KUNDI D, Turkey v Croatia (1700, Parc des Princes, Paris)
KUNDI C, Poland v Northern Ireland (2000, Stade de Nice)
KUNDI C, Germany v Ukraine (2300, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Jumatatu Juni 13
KUNDI D, Spain v Czech Republic (1700, Stadium de Toulouse)

KUNDI E, Republic of Ireland v Sweden (2000, Stade de France, Paris)

KUNDI E, Belgium v Italy (2300, Stade de Lyon)

Jumanne Juni 14

KUNDI F, Austria v Hungary (2000, Stade de Bordeaux)

KUNDI F, Portugal v Iceland (2300, Stade Geoffroy Guichard, St Etienne)

Jumatano Juni 15

KUNDI B, Russia v Slovakia (1700, Stade Pierre Mauroy, Lille)

KUNDI A, Romania v Switzerland (2000, Parc des Princes, Paris)

KUNDI A, France v Albania (2300, Stade Velodrome, Marseille)

Alhamisi Juni 16

KUNDI B, England v Wales (1700, Stade Bollaert-Delelis, Lens)

KUNDI C, Ukraine v Northern Ireland (2000, Stade de Lyon)

KUNDI C, Germany v Poland (2300, Stade de France, Paris)

Ijumaa Juni 17

KUNDI E, Italy v Sweden (1700, Stadium de Toulouse)

KUNDI D, Czech Republic v Croatia (2000, Stade Geoffroy Guichard, St Etienne)

KUNDI D, Spain v Turkey (2300, Stade de Nice)

Jumamosi Juni 18

KUNDI E, Belgium v Republic of Ireland (1700, Stade de Bordeaux)

KUNDI F, Iceland v Hungary (2000, Stade Velodrome, Marseille)

KUNDI F, Portugal v Austria (2300, Parc des Princes, Paris)

Jumapili Juni 19

KUNDI A, Romania v Albania (2300, Stade de Lyon)

KUNDI A, Switzerland v France (2300, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Jumatatu Juni 20

KUNDI B, Russia v Wales (2300, Stadium de Toulouse)

KUNDI B, Slovakia v England (2300, Stade Geoffroy Guichard)

Jumanne Juni 21

KUNDI C, Ukraine v Poland (20000, Stade Velodrome)
KUNDI C, Northern Ireland v Germany (2000, Parc des Princes)
KUNDI D, Czech Republic v Turkey (2300, Stade Bollaert-Delelis)
KUNDI D, Croatia v Spain (2300, Stade de Bordeaux)

Jumatano Juni 22

KUNDI F, Iceland v Austria (2000, Stade de France)
KUNDI F, Hungary v Portugal (2000, Stade de Lyon)
KUNDI E, Italy v Republic of Ireland (2300, Stade Pierre Mauroy)
KUNDI E, Sweden v Belgium (2300, Stade de Nice)

Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Jumamosi Juni 25
Mshindi wa Pili KUNDI A v Mshindi wa Pili KUNDI C (1700, Stade Geoffroy Guichard, St Etienne)

Mshindi KUNDI B v Mshindi wa 3 KUNDI A/C/D (2000, Parc des Princes, Paris)

Mshindi KUNDI D v Mshindi wa 3 KUNDI B/E/F (2300, Stade Bollaert-Delelis, Lens)

Jumapili Juni 26
Mshindi KUNDI A v Mshindi wa 3 KUNDI C/D/E (1700, Stade de Lyon)

Mshindi KUNDI C v Mshindi wa 3 KUNDI A/B/F (2000, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Mshindi KUNDI F v Mshindi wa Pili KUNDI E (2300, Stadium de Toulouse)

Jumatatu Juni 27

Mshindi KUNDI E v Mshindi wa Pili KUNDI D (2000, Stade de France, Paris)
Mshindi wa Pili KUNDI B v Mshindi wa Pili KUNDI F (2300, Stade de Nice)

Robo Fainali
Alhamisi Juni 30

Robo Fainali ya 1, (2300, Stade Velodrome, Marseille)

Ijumaa Julai 1
Robo Fainali ya 2, (2300, Stade Pierre Mauroy, Lille)

Jumamosi Julai 2

Robo Fainali ya 3, (2300, Stade de Bordeaux)

Jumapili Julai 3

Robo Fainali ya 4, (2300, Stade de France, Paris)

Nusu Fainali
Jumatano Julai 6

Mshindi Robo Fainali ya 1 v Mshindi Robo Fainali ya 2 (2300, Stade de Lyon)

Alhamisi Julai 7
Mshindi Robo Fainali ya 3 v Mshindi Robo Fainali ya 4 (2300, Stade Velodrome, Marseille)

Fainali
Jumapili Julai 10

(2300, Stade de France, Paris)