Wednesday, June 15, 2016

EURO 2016: FRANCE 2 v 0 ALBANIA, WENYEJI WASONGA MBELE!

Wenyeji France wamepata ushindi wa 2-0 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakiwa na Mechi 1 mkononi walipoifunga Albania katika Mechi ya Kundi A la EURO 2016 iliyochezwahuko Stade Velodrome, Marseille.
Albania waliwamudu vyema France kwa Dakika 89 na ndipo Antoine Griezmann, alietokea Benchi, kuwatoboa kwa Bao la Kichwa na kwenye Dakika za Majeruhi, Dakika ya 95, Dimitri Payet kufunga Bao la Pili.
Baada ya Mechi 2 France wapo juu Kundi A wakiwa na Pointi 6 wakifuata Uswisi wenye Pointi 4, Romania 1 na Albania 0.