Monday, June 13, 2016

EURO 2016: PIQUE AIPA USHINDI SPAIN!!

BAO la Dakika ya 87 la Gerard Pique limewapa Mabingwa Watetezi Spain ushindi wa 1-0 walipocheza na Czech Republic ya Kundi D la Fainali za EURO 2016 iliyochezwa huko Stadium de Toulouse, Mjini Tolouse Nchini France.
Leo, Spain walimwazisha Kipa wa Manchester United David De Gea Golini badala ya Mkongwe Iker Casillas ikiashiria zama za Casillas ndio baibai na De Gea hakuwaangusha kwa kuokoa michomo miwili mikali hasa mmoja Dakika za mwishoni.

Kama kawaida Spain walitawala lakini ngome ya Czech Republic, ikiongozwa na Kipa wa Arsenal Petr Cech ilisimama imara hadi Dakika ya 87 krosi ya Iniesta ilipounganishwa kwa Kichwa na Pique.