Saturday, June 25, 2016

EURO 2016: POLAND YASONGA ROBO FAINALI KWA PENATI 5-4 DHIDI YA SWITZERLAND

POLAND imeingia Robo Fainali ya EURO 2016 baada ya kuitoa Switzerland kwa Penati 5-4 kufuatia Sare ya 1-1 katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016, iliyochezwa huko Stade Geoffroy Guichard Mjini St Etienne.
Poland ndio walitangulia kwa Bao la Dakika ya 39 la Jakub Blaszczykowski na Switzerland kusawazisha Dakika ya 82 kwa tikitaka ya Xherdan Shaqiri.

Mabao hayo yalidumu hadi Dakika 90 kumalizika na Dakika za Nyiongeza 30 hazikubadili kitu na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati Tano Tano.

Poland walifunga Penati zao zote 5 lakini Switzerland walikosa Penati ya Pili iliyopigwa na Mchezaji Mpya wa Arsenal, Granit Xhaka.

Kwenye Robo Fainali, Poland watacheza na Mshindi kati ya Croatia na Portugal wanaocheza baadae Leo.