Thursday, June 9, 2016

EURO 2016: PORTUGAL YAFANYA MAUAJI! YANYUKA 7-0, RONALDO APIGA 2

PORTUGAL wakicheza Mechi yao ya mwisho ya kujipima kabla kutinga France kwa ajili ya EURO 2016 Jana Usiku huko Estadio da Luz, Lisbon, waliinyuka Estonia Bao 7-0.

Hadi Mapumziko, Portugal waliongoza 3-0 huku Kepteni wao Cristiano Ronaldo akipiga Bao 2 na kupumzishwa wakati wa Haftaimu.

Bao za Portugal zilifungwa na Ronaldo, Dakika za 36, 45, Quaresma, 39, 77, Danilo Pereira, 55, Mets, 61 (alijifunga mwenyewe), na Eder, 80.

Kwenye EURO 2016, Portugal wako Kundi F pamoja na Iceland, Austria na Hungary na wataanza kampeni yao hapo Jumanne Juni 14 kwa kucheza na Iceland.


Baadhi ya Wachezaji wa Portugal wakimpongeza mwenzao Cristiano Ronaldo
Ronaldo akimfunga kwa kichwa kipa wa Estonia
Ronaldo akiteta kwa kitendo kwa mashabiki baada ya kutupia moja ya bao lake