Saturday, June 25, 2016

EURO 2016: WALES WAJIFUNGA BAO! WASONGA ROBO FAINALI

WALES imeingia Robo Fainali ya EURO 2016 baada ya kuitoa Northern Ireland Bao 1-0 katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016, iliyochezwa huko Parc des Princes Mjini Paris.
Bao la ushindi la Wales llilikuwa la kujifunga wenyewe katika Dakika ya 75 na lilianzia kwa Aaron Ramsey aliepenyeza Mpira Winga ya Kushoto na kumkuta Gareth Bale ambae krosi yake ya chini ikatumbukizwa wavuni na Beki wa Northern Ireland Gareth McAuley.

Kwenye Robo Fainali, Wales watacheza na Mshindi kati ya Hungary na Belgium.

VIKOSI:
Northern Ireland (Mfumo 4-5-1):
McGovern; Hughes, McAuley, Cathcart, Jonny Evans; Ward, Davis, Norwood, Corry Evans, Dallas; Lafferty
Akiba: McLaughlin, Ferguson, Baird, McGinn, Grigg, Washington, Carroll, McCullough, McNair, Magennis, Hodson, Mannus.

Wales (Mfumo 3-5-2): Hennessey; Chester, Ashley Williams, Davies; Gunter, Allen, Ledley, Ramsey, Taylor; Vokes, Bale

Akiba: King, Robson-Kanu, Owain Fon Williams, George Williams, Edwards, Richards, Cotterill, Collins, Jonny Williams, Ward, Vaughan, Church.