Tuesday, June 28, 2016

FULL TME: YANGA 0 v 1 TP MAZEMBE

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wakicheza Nyumbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambao ulifurika kupindukia baada ya Mashabiki kuingia bure bila malipo wamepoteza Mechi yao ya pili mfululizo ya Kundi A la Mashindano ya Klabu Barani Afrika ya KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC kwa kupigwa 1-0 na Miamba ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR.

Yanga walianza kwa kufungwa 1-0 Ugenini huko Algeria walipofungwa na MO Bejaia na Mechi yao inayofuata, ikiwa ya 3 kwa Kundi A, ni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam hapo Julai 15 dhidi ya Medeama ya Ghana.
Bao lililoiua Yanga hii Leo lilifungwa Dakika ya 75 na Merveille Bope.
Mechi nyingine ya Kundi A ni Jumatano Juni 29 wakati Medeama wakiwa kwao Ghana kucheza na MO Bejaia ya Algeria.
Kwenye Kundi A, TP Mazembe wako kileleni baada ya kushinda Mechi zao zote mbili wakiwa na Pointi 6 na Yanga wako mkiani wakiwa hawana Pointi.

VIKOSI:
YANGA:
Deo Munishi, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Mahadhi [Geoffrey Mwashiuya, 69’], Obrey Chirwa [Matheo Simon, 71’], Donald Ngoma.

TP MAZEMBE: Sylvain Gbohoud Guelassiognon, Jean Kasusula, Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Rodger Asale, Adama Traore [Deogratius Kanda, 76’], Merveille Bope, Nathan Sinkala, Koffi Christian [Jose Bodibake, 80’], Christian Luyindama, Thomas Ulimwengu.

MSIMAMO: