Monday, June 6, 2016

JAMIE VARDY KUSAJILIWA NA ARSENAL: WAAMBIWA WAFANYE KARAKA KABLA EURO 2016, TOFAUTI NA HAPO HAWAMPATI!

KLABU ya Arsenal imekumbwa na hofu kubwa kwamba wakishindwa kumsaini Straika wa Leicester City Jamie Vardy kabla Mashindano makubwa ya EURO 2016 hayajaanza Wikiendi hii basi upo uwezekano mkubwa sana wa kumkosa kabisa.
Tayari Arsenal washatoa Ofa ya kumnunua Straika huyo wa Mabingwa wa England Leicester City lakini Dili haijakamilika.
Sasa Arsenal wamekumbwa na hofu kubwa kwamba Straika huyo anaweza kupandishwa Dau ikiwa atang’ara akiichezea England kwenye EURO 2016 ambayo ni Mashindano ya Mataifa ya Ulaya yanayoanza Juni 10 huko France.

Jambo hilo litaifanya Arsenal washindwe Bei kumnunua na kutoa mwanya kwa Klabu Tajiri kumnasa.

Msimu huu, Vardy alipiga Bao 24 kwenye Ligi Kuu England wakati Leicester City wakitwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza katika Historia yao ya Miaka 132.