Saturday, June 18, 2016

JUVE WAPIGA HODI EMIRATES KUMNUNUA ALEXIS SANCHEZ

Juventus wanamwania Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez kama mbadala wa Alvaro Morata ambae anatarajiwa kuhama kwa mujibu wa Kituo cha TV cha huko Italy Telelombardia.

Zipo habari nzito kuwa Morata anaweza kurudi Real Madrid ambako aliuzwa kwa Juve Mwaka 2014 kwani Mkataba wa Mauzo yake una Kipengele cha Kumnunua tena kwa Euro Milioni 30.

Kwa mujibu wa Telelombardia Juve tayari wameshaongea na Wakala wa Sanchez, Fernando Felicevich, ili kumnasa Straika huyo kutoka Chile.
Inaaminika, Juve wako tayari kumlipa Mshahara wa Euro Milioni 4.2 kwa Mwaka.
Hivi karibuni, Sanchez, mwenye Miaka 27, alinaswa akinung’unika kukosa Vikombe akiwa na Arsenal na pia kutofanya vizuri kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Sanchez si mgeni kwa Serie A huko Italy kwani alichomoza na kuwika wakati akiichezea Udinese na ndipo Barcelona ikamnunua na kisha kumuuza kwa Arsenal.
Arsenal wanamthamini Sanchez kuwa thamani ya Euro Milioni 55 na ana Mkataba na Klabu hiyo hadi Juni 2018.

Msimu uliokwisha Mei, Sanchez alifunga Bao 17 katika Mechi 41 alizochezea Arsenal na pia kutengeneza Goli 11.