Sunday, June 19, 2016

KIBADENI KUENDELEA KUIFUNDISHA RUVU SHOOTING


KOCHA Mkuu wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni ‘King’ amesema ataendelea kukinoa kikosi katika msimu wa 2016/17.
JKT Ruvu ambayo ilinusurika kushuka daraja msimu uliopita amesema kwa sababu uongozi wa JKT Ruvu bado unamwihitaji ataendelea kuifundisha.
“Nitaendelea kuwa kocha wa JKT Ruvu kwa sababu wao wenyewe wamesema wanahitaji niendelee kwa hiyo sijawakatalia.” anasema Kibadeni
Pia Kibadeni amesema aliandaa ripoti yake vizuri na kuoanisha vitu gani vinatakiwa vifanyiwe kazi ili timu ifanye vizuri katika msimu huu ili yasiwakute yaliyotukuta msimu uiliopita kwani waliponea kushuka daraja.
Katika msimu ujao Kibadeni amesema anahitaji kuona timu hiyo ikishinda mataji na si kupambana kutoshuka daraja.
“JKT si taasisi ndogo inaweza ikazizima Simba na Yanga kama wataungana kwani ina wachezaji wengi na nimewaambia, kuwa na timu sita za JKT haitakuwa na maana bali waunde timu nzuri ambayo inaweza ikapambana kugombea mataji si kupambana kutoshuka daraja”, alisema Kibadeni
Kibadeni ni kocha mkongwe mwenye sifa za pekee kuanzia anacheza hadi kufundisha kwani aliiongoza Simba kufika fainali ya mashindano ya Afrika (CAF) mwaka 1993 pia amewahi kuiongoza Moro United kufika fainali ya michuano ya CECAFA ‘Kagame Cup’ 2006.