Saturday, June 4, 2016

KLABU YA MAN UNITED KUKAMILISHA KUMSAINI ZLATAN IBRAHIMOVIC

Manchester United wanatarajiwa kukamilisha kumsaini Zlatan Ibrahimovic kabla kuanza kwa EURO 2016 Wikiendi ijayo.
Kwa mujibu wa taarifa za Sky Sports hivi sasa Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Man United Ed Woodward na Wawakilishi wa Ibrahimovic wanakamilisha vipengele vya Mkataba wa Mwaka Mmoja ambao Straika huyo wa Sweden atapewa.
Ibrahimovic atahamia Man United kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Paris Saint-Germain kukamilika Msimu huu.


Meneja mpya wa Man United Jose Mourinho amependekeza Ibrahimovic awe Straika wao mkuu akisaidiwa na Chipukizi Marcus Rashford, Anthony Martial na Kepteni Wayne Rooney.

Ibrahimovic amewahi pia kuzichezea Klabu za Malmo FF, Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona na AC Milan na mwenyewe anawania kutwaa Taji la Ubingwa wa Ligi Kuu England kama vile kwenye Ligi za Spain, La Liga, huko Italy Serie A, Ufaransa Ligi 1 na Udachi Eredivisie.