Tuesday, June 21, 2016

LEICESTER WAMNASA SENTAHAFU WA SPORTING GIJON LUIS HERNANDEZ

Leicester wamemsaini Sentahafu Luis Hernandez kwa Mkataba wa Miaka Minne baada ya Mkataba wake na Sporting Gijon ya Spain kumalizika.
Hernandez, mwenye Miaka 27, atajiunga na Mabingwa hao wa England Julai Mosi.
Hernandez, ambae ni Raia wa Spain mwenye Urefu wa Futi 6, alianzia Soka lake akiwa Mwanafunzi kwenye Chuo cha Soka cha Real Madrid.
Beki huyo ameichezea Gijon Mechi 140 na Msimu uliopita alisaidia kuwaponya kushuka Daraja baada ya kuifunga Villareal 2-0 katika Siku ya mwisho ya La Liga.

Kusainiwa kwa Beki huyu kumethibitishwa na Leicester ambao wametoa taarifa kwenye Tovuti yao ambayo imesisitiza kuchukuliwa kwa Hernandez ni kuwaongezea nguvu kwenye Msimu wao wa kwanza kabisa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI.

Mchezaji huyu anakuwa Mchezaji wa Pili mpya kusainiwa na Bosi wa Leicester, Claudio Ranieri, katika kipindi hiki na wa kwanza ni Kipa wa Germany Ron-Robert Zieler aliesainiwa kutoka Hannover.